Wednesday, July 2, 2008

Side B ya Banana!


Side B ya Banana!
Msanii na mmiliki wa B-Band,Banana Ali Zorro, ameamua kuweka wazi upande wa pili wa vipaji vyake.
Nasema upande wa pili kwasababu msanii huyu ameibukia kwenye filamu na ataonekana hivi karibuni katika filamu iliyopewa jina la HANDSOME.Akihojiwa kwenye kipindi cha Nani ni Nani kinachorushwa na siku ya jumamosi televisheni ya Chanel Ten, Banana alisema kuwa ndani ya filamu hiyo pia kutakuwepo na nyota wengine wa filamu kama vile Tea,Adam wa fake pastors,Shumileta na wengineo .Filamu hiyo inaelezea namna kijana anavyoanza maisha yakiwemo ya umaarufu na kuanza kubadilika na muonekano wake katika jamii na mambo yanayowatokea.

Mganda aukwaa UFame! Jumatano, Julai 2, 2008



Mganda aukwaa UFame!
Mwanadada Esther Nabaasa kutoka kwa majirani zetu wa Uganda, ndiye aliyetwaa rasmi tita la cha Sh milioni 85 kwenye shindano la Tusker Project Fame lililomalizika mwishoni mwa wiki jijini Nairobi..baada ya kunguruma kwa miezi kadhaa.
Kwa ushindi huo mwanadada huyo alijinyakulia milioni S za Kenya na mkataba wa kutengenezewa albamu na kampuni kubwa ya kurekodi ya Galo iliyoko Afrika Kusini.Nafasi ya pili ilikwenda kwa Wendy Kimani wa Kenya ambaye alijipatia shilingi milioni 2.5 za Kenya. Katika hatua hiyo ya mwisho iliyokusanya maelfu ya mashabiki ukumbini, washiriki wanne waliobaki walipanda jukwaani na kuimba nyimbo tatu kila mmoja.Washiriki wengine wawili wa kiume, David Ogola na Victor Asava walishindwa kuimba katika hatua hiyo. Baada ya kila mshiriki kuimba wimbo mmoja, msanii kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya 'AY' alipanda jukwaani na kutoa burudani kwa kuimba wimbo wake wa Usijaribu, ambao ulipokelewa kwa shangwe na mashabiki.Kumalizika kwa zamu ya AY, washiriki walipanda tena jukwaani kuimba nyimbo zao za pili, David akiwa wa kwanza akifuatiwa na Esther, Victor na Wendy, kabla ya msanii nyota kutoka Uganda, Bobby Wine naye kupanda jukwaani.Baadaye, MC wa shughuli hiyo, Gaitano Kagwa kutoka Kenya, aliwaonyesha mashabiki gari maalum lililoingia ukumbini likiwa na kitita hicho cha fedha za zawadi, ambao wanaume wanne waliokuwa wamevalia suti na miwani nyeusi, walipopanda jukwaani wakiwa na begi lenye fedha.

Naombeni Radhi Masela! Profesor J


Naombeni Radhi Masela!
Msanii na mmoja wa waasisi nguli wa muziki wa Hiphop nchini,Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay au Big Daddy kama anavyojulikana na wengine, amewaomba radhi baadhi ya wasanii na wanamuziki wenzake wote, ambao kwa namna moja au nyingine amewahi kuwakosea kwenye shughuli zao za kimuziki.
Prof Jay aliomba radhi hiyo kupitia kipindi cha ‘Hip-Hop Base’ kinachorushwa na Luninga la Channel 5 wiki iliyopita, wakati akijibu swali la mwongozaji wa kipindi hicho, kuhusu malalamiko yanayotolewa na wasanii kadhaa dhidi yake, kuwa huwaringia wanapomwomba kumshirikisha katika track zao. “Ni kweli nimewahi kuitwa na wasanii kadhaa katika shughuli zao, lakini nilishindwa kuhudhuria - wakati mwingine mchakamchaka ndiyo unaonifanya nishindwe kwenda, sikukataa kwa makusudi, huwa napenda nikishirikishwa niwe nimejiandaa vilivyo, naomba waniwie radhi wote niliowakosea,” alisema Profesa Jay. Mwanamuziki huyo ambaye amepata tuzo mbalimbali ikiwamo ya utawala bora, aliyoipata kutokana na albamu yake ya ‘Ndiyo Mzee’ ambayo ilitolewa na Redio One na BBC, aliwataka wasanii na wanamuziki wenzake nchini, kudumisha ushirikiano ili kukuza muziki wao. Aliisifu tuzo hiyo ya Utawala Bora, aliyoipata pamoja na viongozi wengine kadhaa mahiri, akiwamo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Joseph Warioba, na kusema kuwa ilimpa sifa lukuki. Pamoja na mambo mengine, alisema huchukua muda mrefu kutoa albamu, ili aweze kutoa kitu cha uhakika. “Albamu kwangu ni kama nembo, ndo maana huwa natoa albamu baada ya miaka miwili,” alisema mwanamuziki huyo, ambaye albamu zake nyingine ni ‘Jina langu’, ‘Mapinduzi halisi’ na ‘Machozi ya damu’.